Home Kitaifa Mpira maalum umezinduliwa kwa ajili ya Ndondo Cup 2017

Mpira maalum umezinduliwa kwa ajili ya Ndondo Cup 2017

4277
0
SHARE

Ndondo Cup ndio kila kitu kwa sasa kwa upande wa soka la kibongobongo, sasa leo Juni 16, 2017 imezinduliwa mipira maalu m ambayo itatumiwa kwenye mashindano ya msimu huu kuanzia hatua ya makundi inayotarajiwa kuanza kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Kinesi pale Shekilango, Dar.

Mipira hiyo inajulikana kwa jina Rabona imezinduliwa kwenye maskani ya timu bya Stim Tosha pande za Mabibo Sokoni maarufu kama Mahakama ya Ndizi. Mipira hiyo inatengenezwa na kampuni ya vijana wa kitanzania inayoitwa Sports Master ambayo mabali na kutengeneza mipira, inatengeneza vifaa vingine mbalimbali vya michezo.

Commercial Manager wa Sports Master Fadhili Nsemwa alikabidhi mipira kwa Yahaya Momamed ‘Mkazuzu’ mwakilishi wa waandaji wa michuano ya Ndondo Cup na zoezi zima la makabidhiano hayo lilikuwa Live kupitia Clouds TV.

Nsemwa amesema, wameona Ndondo Cup ni fursa kwao na wameamua kujitambulisha kwa watanzania kwamba wao ni kampuni ya kizalendo ya vijana wa kitanzania.

“Sisi kama wadau wa michezo Tanzania tumeona hii ni fursa kwetu kujitambulisha kwa watanzania kwamba sisi ni kampuni ya kizalendo ya vijana wa kitanzania ambao tumekusudia kuleta mapinduzi makubwa kwenye vifaa vya michezo.

“Sasa hivi tumeamua tuanze kwa vifaa vya michezo kwa kuanza na mipira lakini tuna vifaa mbalimbali vya michezo kuanzia mpira wa miguu, basketball netball na michezo mingine hadi ya kuogelea.”

“Msimu huu wa Ndondo tumeona tuanze kwa kutoa mipira halafu kuanzia msimu ujao ndio tutaangalia kuhusu vifaa vingine kama jezi na vitu vingine ambavyo tutaweza kutoa.”

“Mipira hii tumechukua mifano kutoka kwenye mipira inayotumiwa kwenye ligi kubwa duniani kama kama EPL kwa hiyo vifaa vyetu vingi tumekuwa tukivitengeneza kwa kuangalia masoko ya wenzetu na si Afrika pekee .”

“Tumezingatia pia mazingira ya nyumbani ili vifaa vyetu viendane na mazingira tunayoishi. Mipira hii ni ya viwango vya juu sana ina uzito na balance inayostahili kutumiwa na wachezaji wetu.”

Mechi ya ufunguzi hatua ya makundi Ndondo Cup 2017 itapigwa kesho Jumamosi Juni 17 uwanja wa Kinesi, Shekilango kati ya Stim Tosha (Mabibo) dhidi ya Makuburi FC (Tabata).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here