Home Kitaifa Exclusive: Yanga wazungumzia kuhusu kuondoka kwa Ngoma, Msuva, Nyionzima na usajili wa...

Exclusive: Yanga wazungumzia kuhusu kuondoka kwa Ngoma, Msuva, Nyionzima na usajili wa Ajib

25179
0
SHARE

Achana na suala la Emmanuel Okwi kurudi Simba lakini mtaaani habari kubwa nyingine ni kuhusu Ibrahim Ajib kusaini Yanga suala ambalo ni kizungumkuti na kila upande umekuwa ukisema yake kuhusu uhamisho wa Ajib.

Wakati Haji Manara akikanusha usajili wa Ajib kwenda katika klabu ya Yanga, upande wa pili ambao ni Yanga wenyewe walikuwa kimya kuzungumzia hili lakini hii leo shaffihdauda.co.tz na Dauda Tv vilipiga hodi katika makao makuu ya Yanga kutaka kujua masuala ya usajili ndani ya klabu hiyo.

Moja kwa moja tulikutana na katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa tukamuuliza kuhusu Ajibu, “unajua mimi nasikia tu kama ninyi munavyosikia lakini Ajib ni mchezaji mzuri na ndio maana alikuwepo pia katika timu ya taifa na hata sisi anatuvutia” alisema Mkwasa.

Hatukuishia hapo bali tulitaka kujua pia kuhusu Donald Ngoma ambae taarifa zinadai hatarudi tena Yanga lakini Mkwasa alikanusha taarifa hizo na kusisitiza kwamba Ngoma haonekani kwa sababu yuko nje ya nchi .

“Ngoma aliaga anakwenda nchini Zimbabwe na baadae Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya goti lake na akatuahidi kwamba katikati ya mwezi wa sita au mwezi wa saba atarudi akiwa fiti kwa ajili ya kututumikia” alisema Mkwasa.

Kuhusu Msuva kutaka kuondoka Yanga, katibu mkuu wa Yanga amesema kama mchezaji akiondoka na kwenda klabu ya nje baasi ni faida kwa mchezaji binafsi lakini pia kwa taifa kwa ujumla na hawana tatizo kuhusu hilo ila tu utaratibu ufuatwe.

“Mchezaji haombwi kusajiliwa kwa kupitia magroup ya whatsapp bali ni lazima utaratibu sahihi ufuatwe, kuna timu kutoka Morocco na pia falme za kiarabu zinamtaka Msuva na sisi hatuna neno ila tunachosisitiza ni utaratibu tu kufuatwa” alisema Msuva.

Ukitaka kuona full video kati ya Dauda Tv na Mkwasa nenda You Tube andika Dauda Tv na subscribe utaiona Interview nzima.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here