Home Kitaifa Exclusive: Okwi atua  Msimbazi kuziba pengo la Ajib

Exclusive: Okwi atua  Msimbazi kuziba pengo la Ajib

33724
0
SHARE

Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao.

Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. 

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi.

Okwi na akiwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hans Pope
Updates: Muda mfupi uliopita, klabu ya Simba kupitia msemaji wao Haji Manara wamethibitsha Okwi amemwaga wino wa kuitumikia Simba, mkatabawa miaka miwili. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here