Home Kimataifa Wachezaji hawaaminiki, ona hawa walivyokana kauli zao katika usajili.

Wachezaji hawaaminiki, ona hawa walivyokana kauli zao katika usajili.

9289
0
SHARE

Wachezaji ni watu wasioaminika sana, leo wanaweza sema hivi na kesho wakasema vile,na hawaaminiki hata kidogo katika masuala ya usajili, hembu ona wachezaji hawa walivyozikana kauli zao.

Cesc Fabregas. Siku chache kabla ya Fabregas kwenda Barcelona minong’ono ilizagaa kwamba huenda angeondoka lakini wakati akihojiwa na waandishi wa habari Fabregas alisema “Nina furaha kuwa Arsenal na tuna kocha mzuri sana na timu nzuri na nikisema kingine zaidi ya hapo nitakuwa muongo” na mashabiki wa Arsenal wakamuamini lakini siku chache baada ya Fabregas kusema hivyo akahamia katika klabu ya Barcelona.

Luis Suarez. “Sababu ya mimi kusaini mkataba mpya ni kwa kuwa naipenda klabu hii,nina furaha sana hapa na kama sina furaha nisingesaini mkataba huu” hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2013/14 lakini miezi michache baadae akaondoka Liverpool huku ikisemekana kwamba matatizo ya kung’ata na kushambuliwa na vyombo vya habari ilikuwa chanzo cha kuondoka lakini ajabu akasema Barcelona ilikuwa sehemu ya ndoto yake.

Neymar.Alikuwa akitajwa sana kuhamia Real Madrid au Barcelona lakini mwenyewe akasema “sijisikii kucheza Ulaya kwa sasa,sio kwamba naogopa ila nina furaha Santos’ hiyo ilikuwa mwaka 2012 na mashabiki wa Santos wakafurahia sana kauliu ya shujaa wao lakini mwaka mmoja baadae Neymar akahamia Barcelona.

Emmanuel Adebayor. “msimu ujao wa ligi nina uhakika 100% nitakuwa mchezaji wa Arsenal” hiyo ilikuwa mwaka 2008 na dunia ikaamini Adebayor anajifunga Arsenal lakini cha ajabu msimu uliofuata tua Adebayor alihamia Man City.

Cesc Fabregas. Sahau alivyowadanganya mashabiki wa Arsenal akatimkia Barcelona bali safari hii ilikuwa zamu ya Barcelona akawaambia “wakati naondoka Arsenal nilisema siwezi kusaini timu yoyote pale Uingereza na itakuwa hivyo” hiyo ilipunguza tetesi za Fabregas kurudi katika ligi kuu ya Epl lakini huwezi amini baada ya kutoka Barcelona Fabregas alikana kauli yake na akarudi Epl aliko hadi sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here