Home Kimataifa Utata mazishi ya Tiote – familia vs shirikisho la soka Ivory Coast

Utata mazishi ya Tiote – familia vs shirikisho la soka Ivory Coast

15672
0
SHARE

Mwili wa Cheick Tiote umesafirishwa kutoka China mpaka nchini kwao Ivory Coast ambapo shughuli ya mazishi itafanyika ili kumpa pumziko la milele kiungo huyo wa zamani Newcastle. 
Tiote, 30, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Tembo wa Waafrika kilichoshinda ubingwa wa Afrika 2015, alidondoka na kufariki dunia wakati akiwa mazoezini na klabu yake ya China Beijing Enterprises. 

Jumanne iliyopita, alifanyiwa ibada maalum na shughuli ya kumuaga jijini Beijing – tukio liloudhuriwa na familia yake, marafiki na wachezaji wenzake wa sasa na wazamani. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza ni kwamba kumetokea mvutano wa wapi pakwenda kumzika Tiote, familia yake inataka aende kuzikwa kijijini kwao Yamoussoukro lakini shirikisho la soka la Ivory Coast linataka mchezaji huyo azikwe jijini Abidjan. 

Mamia ya watu, akiwemo kocha wa zamani wa Ivory Coast Herve Renard, pamoja na wachezaji wenzake kama Gervinho, Wilfred Bony walikuwepo kuupokea mwili wa Tiote ulipowasili uwanja wa ndege wa Abidjan.  

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here