Home Kitaifa RASMI: Ibrahim Ajibu ametua Yanga

RASMI: Ibrahim Ajibu ametua Yanga

62321
0
SHARE

Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib Migomba ‘miguu ya dhahabu’ rasmi anajiunga na Yanga baada ya klabu yake ya sasa kushindwa kufikia nae makubaliano ya kumbakiza kwenye kikosi.

Taarifa ambazo www.shaffihdauda.co.tz inazo ni kwamba, Ajab na uongozi wa Simba hawakufikia makubaliano hivyo nyota huyo akaamua kwenda upande wa pili (Yanga) ambao nao walikua wanamfukuzia tangu kitambo.

Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe kwenye mtandao huu amesema, walijaribu kukaa na Ajib kwa ajili ya mazungumzo ili andelee kubaki Simba lakini mchezaji huyo hakuonekana kuwa tayari kubaki Msimbazi kutokana na kiwango cha pesa alichokua akikihitaji.

“Tumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana ‘spirit’ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele,” amesema boss huyo.

Jana Jumatano Juni 14, 2017 mtandao huu ulitoa story kuhusu ofa tatu alizokuwanazo Ajib ambazo zilikuwa ni kutoka Simba, Yanga na Singida United ambapo Singida ndio ilikua timu yenye dau refu kuliko Simba na Yanga lakini Ajib alikuwa na wasiwasi kwenda Singida kutokana na kuhofia maisha yake ya baadae katika soka.

Ajib ambaye alianza kutamba Simba akitokea kikosi cha vijana alikuwa mchezaji huru baada ya kuhitimisha mkataba wake ndani ya Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here