Home Kimataifa Mayweather ulingoni tena Las Vegas August 26.

Mayweather ulingoni tena Las Vegas August 26.

3666
0
SHARE

Jimmy Floyd Money Mayweather ni bondia ambae panapokuwa na pesa huwa hawezi kataa kupigana kwani kila mwaka amekuwa akisema anaachana na ndondi lakini linapokuja dau kubwa la ndondi huwa anakubali kurudi ulingoni.

Pambano kati ya Mayweather na Conor McGregor limekuwa likizungumziwa sana japo kuna wakati ilionekana kama jambo hilo halitatokea lakini hatimaye muafaka umefikiwa na sasa Mayweather na McGregor watapanda ulingoni mjini Las Gas.

Mpambano huo utachezwa chini ya sheria za mchezo wa Boxer japokuwa McGregor hajawahi pigana mchezo wa Boxer popote pale lakini yeyey ni mchezaji wa ngumi za Kick Boxer tu na mchanganyiko wa martial arts.

Pambano hilo litamfanya Mayweather kuweka mfukoni kiasi cha zaidi ya $100m lakini tayari wachambuzi wa masuala ya masumbwi wameshaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Mayweather na wengi wanaona kutokana na muda aliokaa nje anaweza kupigwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here