Home Kitaifa Liuzio amezungumzia kuhusu usajili unaofanywa na Simba

Liuzio amezungumzia kuhusu usajili unaofanywa na Simba

9930
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

Juma Liuzio anaecheza kwa mkopo katika klabu ya Simba akitokea Zesco United ya nchini Zambia, amesifu usajili wa timu hiyo kuwa wanaonyesha kwamba wanataka kwenda kushindana katika mashindano ya kimataifa na si kushiriki.

“Simba usajili wanaoufanya mpaka hivi sasa wanaonyesha kabisa kuwa hawaendi kushiriki bali wanaenda kushindana kutokana na kuwa wamesajili wachezaji wazoefu ambao sio wageni kabisa wa mashindano ya kimataifa,” alisema Luizio.

Luizio pia amesema kuwa kuja kwake kumemfanya aongezeke kujiamini kutokana na kupata mechi za mara kwa mara kucheza tofauti na ambavyo ilivyokuwa Zesco licha ya kuwa alikuwa akisumbuliwa na majeraha.

“Simba nimepata nafasi nyingi za kucheza, nimeongeza kujiamini na nina utimamu wa mwili baada ya kucheza hapa tofauti na ilivyokuwa Zesco kwa hiyo kwa hali hii naweza nikacheza sehemu yoyote ile hata ikiwa sio Simba,” alisema Luizio.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here