Home Kitaifa Yanga imemsaini mchezaji wa kwanza kwa ajili ya msimu ujao

Yanga imemsaini mchezaji wa kwanza kwa ajili ya msimu ujao

7933
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

Timu ya Yanga imefanikiwa kumsainisha mkataba beki wa kati kutoka Taifa Jang’ombe inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar. Beki huyo ni Abdallah Haji Shaibu maarufu kwa jina la Ninja.

Mchezaji huyo anakuwa wa kwanza kusaini mkataba kuelekea msimu ujao, katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema, klabu imejiridhisha juu ya ubora wa mchezaji huyo baada ya kupewa taarifa za awali za mchezaji huyo katika soka akiwa huko Zanzibar.

Ninja amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga na klabu ya Yanga, Yanga walikuwa kimya kwenye masuala ya usajili wakati Simba ikitamba katika kusainisha mikataba wachezaji lakini nao wameanza kujibu mapigo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here