Home Kitaifa Nyosso is back, Kagera Sugar imesaini 6 kwa mpigo

Nyosso is back, Kagera Sugar imesaini 6 kwa mpigo

13754
0
SHARE

Juma Nyosso mzee wa kazi anarejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Kagera Sugar ya mjini Bukoba moani Kagera.

Nyosso amemaliza kutumikia adhabu yake ya kutumikia kifungo cha kukaa nje ya uwanja tangu September 2015 alipofungiwa na TFF kutojihusisha na soka kwa miaka miwili kutokana na kitendo cha kumshika John Bocco sehemu za siri wakati wa mchezo wa ligi kuu kati ya Azam dhidi ya Mbeya City.

Kagera Sugar kupitia ukarasa wao rasmi wa Instagram (kagerasugarfootballclub) imetoa taarifa ya kumsaini Nyosso pamoja na wachezaji wengine watano ambao watajiunga na timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha bora wa msimu uliopita Mecky Maxime.

Wachezaji wengine waliosaini mikataba ya kujiunga na Kagera Sugar ni pamoja na Peter Mwalyanzi, Ludovic Venance na Omary  Daga ‘Dagashenko’ wote wakitokea African Lyon ambayo imeshuka daraja.

Peter Mwalyanzi

Wengine ni golikipa wa Hussein Kipao ambaye msimu uliopita alikuwa anacheza JKT Ruvu ambayo pia imeshuka daraja huku mchezaji mwingine akiwa ni mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Japhary Kibaya.

Kagera Sugar inaendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao wa ligi ambapo msimu huu timu ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi pamoja na kutoa washindi wa tuzo binafsi (Maxime-kocha bora, Mbaraka Yusuph-mchezaji bora anaechipukia huku Kaseja akiwa kwenye orodha ya magolikipa watatu waliokuwa wakiwania tuzo ya golikipa bora).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here