Home Kitaifa Machache ya kufahamu kuhusu beki mpya wa Yanga

Machache ya kufahamu kuhusu beki mpya wa Yanga

21680
0
SHARE

Baada tu ya kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga, beki wa kati Abdallah Haji Shaibu alinaswa katika exclusive interview na Sports Extra ya Clouds FM ambapo ametoa historia yake ya soka kwa ufupi pamoja na lini Yanga walianza kumfukuzia.

Ameeleza pia malengo yake binafsi baada ya kujiunga na Yanga huku akimtaja nahodha wa Yanga mzanzibar Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa amechangia kwa kiasi kikubwa yeye kujiunga na mabingwa hao VPL.

Safari yake ya soka ilianzia wapi?

“Nimetoka timu ya Taifa Jang’ombe, nilianza kucheza kwenye timu inaitwa Rioblanco  mwaka 2008 nikicheza kama mshambuliaji na nilikuwa najulikana kwa jina la Benzema, badae nikaenda kucheza D Three mwaka 2010 hadi 2011.”

“Mwaka 2012 Leopard Centre mwaka 2011/2012 baada ya hapo nikaenda kucheza timu ya daraja la pili taifa timu inaitwa Danger ipo maeneo ya Daraja Bovu Zanzibar nikaipandisha daraja la kwanza, bahati nzuri nikajiunga na timu ya Taifa Jang’ombe mwaka 2014 hadi najiunga na Yanga.”

Kumbe Yanga wameanza kumfukuzia kitambo tu!

“Kwa sasa nacheza nafasi ya beki wa kati, Yanga wameanza kunifatilia kitambo, kuna mwaka tulicheza nao kwenye kombe la Mapinduzi wakati huo nilikuwa nacheza ligi daraja la pili na timu ya Taifa Jang’ombe nikasikia fununu kwamba wananihitaji lakini zilikuwa ni habari ambazo hazina uhakika.”

“Hata mwaka huu wakati wa mashindano ya Mapinduzi nilisikia viongozi wa Yanga walikuwa wanataka namba yangu ya simu nikawapa na leo hii nimekuja kujiunga na Yanga.”

Anasemaje kuhusu uwezo wake wa kuitumikia Yanga?

“Naamini ninauwezo wa kucheza Yanga na kwauwezo wa Mungu atanisaidia huku mimi mwenyewe nikipambana ili kufanya vizuri.”

Cannavaro amehusika na ujio wake ndani ya Yanga?

“Cannavaro kanishawishi sana mimi kujiunga Yanga, sijawai kuzungumza nae lakini hata kwenye account zangu za mitandao ya kijamii nilikuwa nikimpost sana kwa sababu ninakubali huku nikiamini kuna siku nitakuja kucheza katika level yake au zaidi yake.”

Baada ya kufanikiwa kuingia Yanga, nini malengo yake…

“Malengo yangu nikiwa Yanga kwanza nataka kuifikisha timu nzuri zaidi halafu malengo yangu binafsi ni kufika mbali zaidi ya hapa Yanga.”

Kuhusu changamoto ya kupata nafasi kikosi cha kwanza je?

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata nafasi kwenye kikosi cha Yanga na kwa uwezo wa Mungu nitapata nafasi ya kucheza.”

Ukianchana na Yanga, ni timu gani nyingine zilikuwa zinamnyatia? 

“Mbeya City, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kulikuwa kuna mazungumzo lakini yalikuwa ni ya juujuu wengine walikuwa wanazungumza na viongozi wa timu yangu.”

Shaibu anaingia kwenye kikosi cha Yanga na kukutana na Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Vicent Andrew na mkongwe Cannavaro wote wakicheza kama walinzi wa kati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here