Home Kitaifa Kikosi cha Mbao kinabomoka, viongozi wanajuta

Kikosi cha Mbao kinabomoka, viongozi wanajuta

14015
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu

UONGOZI wa klabu ya Mbao umelazimika kuanza upya kukisuka kikosi chao mara baada ya nyota wake muhimu wote wa kikosi cha kwanza kutimka na kujiunga na timu nyingine, huku wengine wakiwa bado wanafanya mazungumzo na timu za ligi kuu huenda nao wakaondoka siku za hivi karibuni.

Viongozi wa Mbao FC wamekiri kuwa walifanya makosa kwa kuwasainisha wachezaji wao mikataba mifupi (mwaka mmoja) hiki kitendo ambacho kimepelekea wachezaji wote tegemeo kuondoka wakiwa huru.

Simba ndio klabu ya kwanza kuvuja ukuta wa Mbao baada ya kumsainisha aliye kuwa beki wa kushoto wa timu hiyo, Jamal Mwambeleko ambae pia alikuwa katika mapendekezo ya kocha wa Yanga, George Lwandamina.

Azam nayo haikuwa nyuma ya Simba na kujiingiza mkukumkuku na kuwasainisha nyota wawili wa Mbao ambao ni Salmin Hoza na Benedict Haule, na utambue kwamba Hoza ni kiungo mahiri ambae Yanga nao walikuwa wakimtumbulia macho lakini wameshindwa kupata saini ya kiungo huyo.

Wakati Yanga wakimlalamikia meneja mkuu wa Azam, Abdul Mohammed alivyowapiku na kuinasa saini ya kiungo huyo, matajiri hao wa ligi kuu walionesha ubabe wao baada ya kumsainisha Haule ambae nae kuondoka kwake kunaifanya Mbao kuendelea kubomoka zaidi.

Lakini pia Simba na Yanga bado zina pigana kuwania saini ya beki wa kati wa Mbao, Yusuph Ndikumana ambae mkataba wake umemalizika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here