Home Kimataifa Tetesi za usajili Jumanne ya leo, Ranieri apata timu mpya.

Tetesi za usajili Jumanne ya leo, Ranieri apata timu mpya.

8111
0
SHARE

Baada ya kuipandisha ligi kuu kocha Claudio Ranieri aliipa Leicester ubingwa wa Epl lakini msimu uliofuata alitimuliwa na timu hiyo, lakini leo kocha Claudio Ranieri amepata klabu mpya baada ya timu ya Nantes ya nchini Ufaransa kumtambulisha kama kocha wao mpya.

Lakini huko huko nchini Ufaransa klabu ya Psg imeionya klabu ya Barcelona kuhusu kiungo wao Marco Veratti na kusisitiza kwamba kiungo huyo hauzwi kwa dau lolote hivyo Barcelona wakatafute mchezaji mwingine.

Klabu ya Arsenal ambayo inamsaka kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, sasa klabu ya Lyon imetaja dau ambalo Arsenal wanapaswa kulipa kama wanamtaka itabidi watoe euro 48.7m.

Baada ya kutoswa na kocha George Sampaoli aliyepata kazi mpya ya kuinoa timu ya taifa ya Argentina, klabu ya Sevilla leo imepata kocha mpya ambapo aliyekuwa kocha wa Celta bwana Edurdo Berizzo amepewa jukumu hilo la Sampaoli.

Mshambuliaji raia wa Crotia Ivan Perisic ambaye anawindwa sana na klabu ya Manchester United inasemekana amewaambia wazi waajiri wake klabu ya Inter Milan kwamba wamuache ajiunge na Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here