Home Kitaifa Mkasa wa Juma Kaseja kuhama Simba kwenda Yanga mwaka 2008

Mkasa wa Juma Kaseja kuhama Simba kwenda Yanga mwaka 2008

4551
0
SHARE

Golikipa wa Kagera Sugar Juma Kaseja amefafanua ni kipi kilichomfanya atoke Simba mwaka 2008 na kujiunga na mahasimu wao Yanga huku akiwa ni mchezaji aliyecheza katika timu hizo mara mara mbili (kwa kila timu) kwa nyakati tofauti.

“Mara ya kwanza natoka Simba 2008 hadi naenda kusaini Yanga nilikuwa naongea na viongozi wa Simba. Nipo na viongozi wa Yanga lakini nilikuwa nawaambia subirini kidogo natoka nje naenda kuongea na viongozi wa Simba.”

“Nawaambia viongozi wa Simba nimepewa dola 30,000 mwaka 2008 ilikuwa ni sawa na milioni 36 ambapo kwa Tanzania ndio nilikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa pesa nyingi, nilikuwa nawauliza nyinyi mnaweza kunipa hiyo hela? Lakini kuna watu walikuwa wananiambia chukua hiyo pesa sisi hatuna uwezo wa kukupa, wapo mpaka leo hii ndani ya Freinds of Simba ambao ndio wanaoongoza Simba sasa hivi.”

“Wananiambia kila siku ulikuwa unatupigia kelele tukutafutie timu uende ukacheze nje, sasa hiyo pesa ni sawa na nje chukua.”

“Lakini mimi nawashukuru kwa sababu kama wangekuwa na roho mbaya leo hii labda nisingekuwa na maisha haya niliyonayo sasa hivi. Walinitia ujasiri kwa sababu nilikuwa na hofu ya kutoka upande mmoja kwenda mwingine kwamba nitaishije lakini nikaenda nikacheza.”

“Kingine kilichonifanya niende ni zile shutuma nilizokuwa napewa kwamba nawauzia Yanga mechi, nikiwa nataka kuwaminisha kwamba kama huwa nawauzia Yanga wananiamini vipi nikacheze kwao. Wakati nipo Yanga nikawa naambiwa wewe ni Simba, Simba nao wananiambia mkataba wako ukiisha urudi, basi mkataba ulivyoisha nikarudi tena Simba.”

“Nilivyorudi Simba, yakaanza tena manen kwamba nakula hela Yanga, nikakaa nusu msimu sichezi. Yanga wakaja wakanipa mzigo milioni 40 niakaenda tena Yanga. Haya mamo ya kuambiwa nakula hela ndio yalikuwa yanachangia mimi kuhamahama kwenye timu hizi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here