Home Kitaifa Maoni ya Kaseja baada ya John Bocco kuondoka Azam

Maoni ya Kaseja baada ya John Bocco kuondoka Azam

13929
0
SHARE

Juma Kaseja anaamini wachezaji waandamizi hawapewi heshima wanayostahili kwenye vilabu vyao licha ya kujitolea na kuvitumikia vilabu hivyo kwa moyo ndio maana wachezaji waliodumu kwa muda mrefu wanaendelea kuvikimbia vilabu vyao.

Hiyo imekuja baada ya klabu ya Azam kumtosa aliyekuwa nahodha wao John Bocco kufuatia mkataba wa mchezaji huyo kumalizika. Lakini habari za chinichini zinadai kwamba, Azam na Bocco hawakuelewana kuhusu mambo maslahi ambapo mchezaji huyo alikataa dau la klabu hiyo ambalo lilikuwa dogo kwake kwa ajili ya kusaini mkataba ili aendelee kuitumikia klabu hiyo.

“Sijui kuna nini kimetokea ndani ya Azam kwa sababu hata mimi nasikia tu kama mnavyosikia ninyi kwamba, kuna utaratibu umewekwa hakuna kusajili mchezaji kwa zaidi ya milioni 15 lakini tunasikia Mbaraka kachukua zaidi ya mioni 15 sasa mimi nadhani kuna vitu vimetokea kwenye mpira wa Tanzania kwa kutaka kuwaondoa wachezaji waandamizi kwenye timu na hivi vitu havipo Azam tu, vipo kwenye mpira wa Tanzania, Azam wamevitoa kwenye hizi timu mbili na kuvipeleka kwao.”

“Watu hawataki kuwapa heshima, lazima wawape heshima wachezaji, Bocco ni mchezaji mkubwa ndani ya Azam wanatakiwa wampe heshima yake. Hata kama kulikuwa na matatizo ya mambo ya hela na uchumi wangekaa chini wazungumze nae, Bocco na yeye ni binadamu kama miaka yote kachukua pesa nyingi anawezaje kukataa kwa mwaka mmoja kama ameeleweshwa¬† kuwa timu haiku vizuri kuhusu hali ya timu kiuchumi?”

“Lakini kwa mchezaji kama Bocco ambae ameshajitolea sana kwenye timu hata yeye hawezi kuwa na furaka kwa sababu anaona kama amedharaulika na hivyo ni vitu ambavyo wamefanyiwa watu wengi sema kwa Azam ndio mchezaji wa kwanza lakini kwenye hizi timu nyingine watu wamefanyiwa sana.”

Bocco amesha saini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba kuanzia msimu ujao wa 2017/2018.k

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here