Home Kitaifa Kiduku ameeleza Julio alivyomtoa Ndondo Cup hadi VPL

Kiduku ameeleza Julio alivyomtoa Ndondo Cup hadi VPL

6006
0
SHARE

Kelvin Sabato ‘Kiduku’ ni miongoni mwa wachezaji walioibuliwa na michuano ya Ndondo Cup, mchezaji huyo amemshukuru kocha wa zamani wa Mwadui Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwa kumwamini na kumtoa kupitia Ndondo hadi ligi kuu Tanzania bara.

Kiduku amesimulia namna Julio alivyomchukua kumpeleka Mwadui FC ambapo kwa sasa anacheza Majimaji alikosajiliwa akitokea Stand United ya mkoani Shinyanga.

“Namshukuru sana kocha Julio, siku hiyo nilikuwa na timu yangu Abajalo mara Julio akatokea pale uwanja wa Makurumla akaniona siku hiyo nafanya shughuli zangu, niliwapiga goli mbili Sharifu Shamba Julio akasema hiki kidume siwezi kukiacha akanibeba.”

“Akajaribu kunipenyeza kwenye timu ya ‘Serengeti Maboresho’ enzi hizo, alimtafuta Kim Polsen wakati huo alikuwa ndio kocha mkuu, akasema hawezi kunitangaza kwa sababu hajaniona kwa hiyo akaagizwa nipelekwe.”

“Nilipofika kule kila nikifanya mazoezi mambo yanajipa tu kwa sababu haya mandondo  nayo yanafanya tujiamini, sasa Kim akawa anasema njoo  kesho lakini kwa bahati mbaya nilichana nyama za paja kwenye mazoezi ya mwisho wakati huo nimeshapewa taarifa kwamba nipo kwenye hesabu za ma-striker wa Kim.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here