Home Kimataifa Cheikh Tiote amuingiza matatani mchezaji mwenzake aliyeko jela.

Cheikh Tiote amuingiza matatani mchezaji mwenzake aliyeko jela.

4795
0
SHARE

Wiki iliyopita dunia ilikumbwa na msiba mkubwa katika soka baada ya kumpoteza kiungo wa zamani wa Newcastle na timu ya taifa ya Ivory Coast Cheikh Tiote aliyefariki nchini China alipokuwa akicheza soka baada ya kuanguka akiwa katika mazoezi.

Sasa kuna mchezaji anaitwa Nile Ranger ambaye ameshawahi kucheza pamoja na Tiote katika klbu ya Newcastle, Nile Ranger yuko gerezani akiwa anatumikia kifungo cha miezi 8 na sheria zinasema unapokuwa mfungwa huwezi kutumia mitandao ya kijamii wala simu.

                         

Lakini wiki iliyopita baada ya Tiote kufariki ukurasa wa Instagram wa Nile Ranger ulipost picha ya Tiote na kuandika ujumbe unaoonesha kuumizwa na kifo hicho “alikuwa mtu shupavu sana,imara sana na mwenye weledi wa hali ya juu, naipa pole faimilia yake” iliandika sehemu ya ujumbe wa Ranger.

Msemaji wa gereza alilopo Ranger nchini Uingereza amesema bado hawana uhakika wa nani kapost ujumbe huo lakini wanashirikiana na polisi kupeleleza suala hilo na kusisitiza kwamba halikubaliki na watachukua hatua kali sana kwa Ranger akibainika kuhusika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here