Home Ligi EPL #DTU: Madrid kutumia fedha za Morata na James kumsajili Mbappe

#DTU: Madrid kutumia fedha za Morata na James kumsajili Mbappe

16967
0
SHARE

Hatma ya James Rodríguez inaonekana kuelekea Kusini Magharibi mwa Jiji la London baada ya Chelsea kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania saini ya mchezaji huyo. 

Kulikuwa na tetesi za mcolombia huyo kujiunga na The Blues wakati Oscar alipojiunga na Shanghai SIPG katika dirisha la usajili la January lakini aliamua kubaki Bernabeu kupigania nafasi yake. 

Hivi sasa, Chelsea ikiwa ina tiketi ya makundi ya UCL 2017/18, Antonio Conte anahitaji kukiimarisha kikosi chake ili kuweza kuhimili ushindani msimu ujao. 

Inaripotiwa kocha huyo muitaliano ameshaamua kwamba Diego Costa na Cesc Fabregas sio miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye mipango na ameshaomba usajili wa James na Alvaro Morata ambaye tayari ameshapoteza matumaini ya kumpata baada ya dalili zote kuonyesha anaelekea Old Trafford – na sasa inaelezwa amewekeza nguvu katika kupata saini ya James Rodriguez. 

Inaaminika Real Madrid wamejipanga kupata fungu €130m kutokana na mauzonya wachezaji hawa wawili na watatumia fedha hizo kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, japokuwa ripoti zinaeleza kwamba mchezaji huyo huenda akabaki Ligue 1 kwa angalau msimu mmoja. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here