Home Kimataifa Ujerumani waisulubu San Marino, huku Lewandoski akifunga hattrick.

Ujerumani waisulubu San Marino, huku Lewandoski akifunga hattrick.

2977
0
SHARE

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kikiwa nyumbani waliikaribisha timu ya taifa ya San Marino katika mchezo ambao San Marino waliishia kudhalilika baada ya kupewa zigo la mabao saba kwa nunge kutoka kwa vijana hao wa Joachiem Low.

Alianza Julian Draxler dakika ya 11 kuishushia kipondo San Marino na baadae Sandro Wagner akfunga mara mbili na Amin Younes akafunga mara moja na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko Ujerumani wakiongoza mabao manne kwa sifuri.

Kipindi cha pili mlinzi wa klabu ya Arsenal Shkordan Mustafi alifunga bao la 5, Julian Brandit akafunga la 6 kabla ya Sandro Wegner kufunga bao lake la 3 katika mchezo huo na la 7 kwa timu ya taifa ya Ujerumani, lakini kule Norway nako timu yao ya taifa ilitoka sare ya moja moja na Czech Republic.

Montenegro nao walikuwa nyumbani kuikaribisha Armenia ambapo Montenegro waliibuka kidedea kwa kuibamiza Armenia jumla ya mabao manne kwa  huku Steven Jovetic akiifungia Montenegro hat trick na lile lingine likiwekwa kambani na Fatos Beciraj na la Armenia likifungwa na Rusian Koryan.

Poland nao wakiwa nyumbani waliikaribisha Romania ambapo katika mchezo huo mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Robert Lewandoski aliibuka shujaa wa Poland baada ya kufunga mabao yote matatu na lile la kufutia ,achozi la Romania likifungwa na Bogdan Stancu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here