Home Kimataifa Jelena Ostapenko ashinda French Open akiwa na miaka 20 tu.

Jelena Ostapenko ashinda French Open akiwa na miaka 20 tu.

1207
0
SHARE

Siku ya Alhamisi ya tarehe 8 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwanadada Jelena Ostapenko kutoka Latvia ambapo alikuwa akitimiza umri wa miaka 20 umri unaoonekana mdogo tofauti na kile ambacho amekifanya siku ya leo katika mashindano ya French Open.

Jelena Ostapenko leo ameingia katika vitabu vya mchezo wa tennis baada ya kutoka nyuma kwa seti 3-0 na baadae kuibuka kidedea kwa ushindi wa seti 4-6,6-4,6-3 dhidi ya mwanadada mwingine anayekuja juu katika mchezo huo Simonna Help kutoka nchini Romania.

Tofauti na Simonna Help ambaye hii ilikuwa mara yake ya pili kushiriki fainali za michuano mikubwa kama French Open lakini kwa Jelena hii ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki fainali za michuano mikubwa kama hiyo huku akishikilia nafasi ya 47 katika viwango vya tennis.

Kutokuwepo kwa Serena Williams katika fainali hiyo kulimfanya Simmona kupewa nafasi kubwa kuibuka bingwa wa michuano hiyo na tofauti na matarajio ya wengi Help amekosa tena ubingwa huo na katika mchezo huo mashabiki wengi wa Romania waliamini Simonna anaweza kufanya kile alichofanya katika michezo yake 6 iliyopita lakini hali ikawa tofauti.

Baada ya mchezo huo Jelena Ostapenko amesema haamini hata kidogo kama ameshinda French Open “hakika na umri kama wangu siamini hata kidogo kama nimeshinda taji hili” kwa upande wa Simmona alimpongeza Ostapenko kwa ushindi huo na kukiri kwamba amesikitika sana kutochukua ubingwa huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here