Home Kimataifa Harry Kane aiokoa Uingereza.

Harry Kane aiokoa Uingereza.

3099
0
SHARE

Timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa nchini Scotland leo kukabiliana na wenyeji wao hao wa Scotland, mchezo huo kati ya Uingereza na Scotland ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani wote wawili walihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki kombe lijalo la dunia.

Uingereza walitangulia kufunga kupitia kwa Oxlade Chamberlain dakika ya 70 lakini ilipofika dakika ya 87 Scotland walisawazisha bao hilo kupitia kwa Leigh Griffiths na dakika ya 90 akafunga lingine, watu wakiamini Scotland wangeshindfa mchezo huo Harry Kane aliisawzishia timu ya taifa ya Uingereza dakika ya 90.

Katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Slovenia walikuwa nyumbani kuikaribisha Malta ambapo mabao ya Josip Ilicic na Novakovic yalitosha kuimaliza Malta na wenyeji wa mchezo huo wakaibuka kidedea kwa ushindi huo wa mabao mawili kwa sifuri.

Kazakhstan nao walikuwa nyumbani kuikaribisha timu ya taifa ya Dernmark ambapo katika mchezo huo ambao Kazakhstan walilazimika kumaliza pungufu baada ya Islamakhan kupewa kadi nyekundu dakika ya 43 wwalipoteza kwa kipigo cha mabao matatu kwa moja.

Northen Ireland nao walikuwa ugenini kukabiliana na timu ya taifa ya Azerbaijan na Northen Ireland kuibuka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa sifuri bao likifungwa dakika ya 90 na Stuart Dallsas.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here