Home Kimataifa Siku za Bradley Lowery kuishi zimekaribia kuisha, Defoe akosa neno.

Siku za Bradley Lowery kuishi zimekaribia kuisha, Defoe akosa neno.

10198
0
SHARE

Unamkumbuka Bradley Lowery yule dogo shabiki mkubwa wa Stoke City anayesumbuliwa na kansa? sasa taarifa kutoka kwa mama yake mzazi zinasema bado wiki chache tu tumpoteze Bradley kutokana na ugonjwa huo ambao madaktari wameshindwa kuutibu.

Kila mpenda soka habari hizi zinamtia simanzi lakini mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Jermain Defoe hakika anapitia wakati mgumu sana kutokana na habri hizi na amekiri kupatwa na simanzi kubwa.

Inafahamika kwamba Defoe na Bradley walikuwa na uhusiano mkubwa sana ndani na nje ya uwanja na baada ya mama mzazi wa Bradley kutoa taarifa hizo imemfanya Defoe kuipigia simu familia ya Bradley kila aamkapo.

“Kila asubuhi inapofika nalazimika kumpigia simu mama yake na huwa ananiambia wako poa, ila nakosa hata maneno ya kuongea kutokana na habari za Bradley kubakisha siku chache za kuishi dunia” alisema Defoe.

Defoe ambaye atahamia katika klabu ya Bournamouth hivi karibuni tayari ameshaanza kukumbuka nyakati za furaha alizopitia na Bradley na anatamani Bradley aendelee kuwepo katika mechi zake zijazo jambo ambalo ni gumu.

Bradley amekuwa akijitokeza sana katika michezo ya Sunderland ili kumpa support Jermain Defoe lakini pia mwezi March mwaka huu alikuwepo katika dimba la Wembley wakati England walipocheza na timu ya taifa ya Lithuania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here