Home Kimataifa Real Madrid wakataa “vipesa” vya United kwa ajili ya mchezaji huyu.

Real Madrid wakataa “vipesa” vya United kwa ajili ya mchezaji huyu.

7390
0
SHARE

Vita kati ya Real Madrid na Manchester United katika usajili imechukua sura mpya baada ya Real Madrid nao kulipiza kile ambacho Manchester United waliwafanyia kwa mlinda lango wao David De Gea.

Wiki iliyopita kuliibuka taarifa kwamba Real Madrid walijaribu kutuma ofa kwa Manchester United kwa ajili ya De Gea lakini United waliikataa ofa hiyo na kuwaambia Real Madrid wakaongeze dau hadi euro 66m.

Sasa wiki hii nayo United wametuma ofa kwa Real Madrid kujaribu kumsajili mshambuliaji wao Alvaro Morata ambaye tayari amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kocha Zinedine Zidane.

Manchester United wametuma ofa ya euro 52m lakini Real Madrid wamekataa kiasi hicho cha pesa na kuwaambia wakaongeze tena euro 26.6m ili kumpata Alvaro Morata ambaye pia anafukuziwa na Chelsea na Ac Millan.

Kutokana na ukubwa wa kikosi cha mabingwa hao wa champions league na kutokana na dakika chache ambazo Morata amekuwa akizipata uwanjani ni wazi kwamba Mhispania huyo anataka kuondoka ili kwenda sehemu ambako anaweza kupata nafasi ya kucheza.

Jose Mourinho anapambana sana kutafuta mshambuliaji mkubwa lakini madau yao yamekuwa hayashikiki, Mourinho anamtaka Lukaku pia ambaye habari zinadai anarudi Stamford Bridge lakini pia Mourinho anafuatilia kwa makini sahihi ya Andrea Belotti wa Torino.

Bado haijfahamika kama Jose Mourinho bado atatuma ofa nyingine kwa Real Madrid au ataachana na mpango wa kumnunua Morata au labda huenda akamtumia David De Gea kama sehemu ya kumnasa Alavaro Morata.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here