Home Kimataifa Hapa ndipo Mario Balotelli atakapocheza msimu ujao.

Hapa ndipo Mario Balotelli atakapocheza msimu ujao.

27744
0
SHARE

Baada ya matatizo mengi na kiwango kushuka sana, hatimaye mshambuliaji mtukutu wa klabu ya Nice Mario Balotelli amekuwa na msimu bora sana tangu ajiunge na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ufaransa.

Baada ya Balotelli kuonekana bora akiwa na Nice tayari vilabu mbalimbali vya barani Ulaya vimeshaanza kupiga hodi nchini Ufaransa ili kujaribu kutafuta saini ya mshambuliaji huyo kutoka Italia.

Uzuri wa Balotelli ni kwamba wakala wake ni wakala ambaye anajua haswa kucheza na akili za vilabu vikubwa barani Ulaya pale anapotaka kumuuza mchezaji wake, wakala wa Mario ndio wakala aliyemuuza Paul Pogba kwenda Manchester United bwana Mino Raiola.

Wakati Las Palmas ya Hispania, Besitikas ya Uturuki, na Napoli ya Italia wakiendelea na mpambano wa kutafuta saini ya Balotelli tayari Raiola ameshajua mahalia ambapo Balotelli anakwenda kucheza na amepaweka wazi.

Waandishi wa habari nchini Ujerumani walikusanyika katika mkutano wa klabu ya Borussia Dortmund ilipokuwa ikimtangaza kocha wao mpya  Peter Bosz na Raiola bila kutarajiwa alijitokeza katika mkutano huo.

Raiola alipoulizwa kuhusu Mario Balotelli akaweka wazi kwamba “atacheza hapa Borussia Dortmund”, kutokana na kauli hiyo ya Raiola huenda labda Dortmund wameamua kumchukua Balotelli kuziba nafasi ya Pierre Aubameyang ambaye inasemekana anaelekea Ufaransa kukipiga PSG.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here