Home Kimataifa Habari za usajili zilizovuma leo Jumatano.

Habari za usajili zilizovuma leo Jumatano.

10540
0
SHARE

Habari za chinichini zinadai kwamba klabu ya Arsenal wameshindwana na Alexis Sanchez kuhusiana na suala la mkataba mpya na sasa mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester City ambao wameshafanya mazungumzo naye ya chini chini.

Manchester United nao kwa upande wao inaonekana ni kama wameshashinda vita ya kumbakiza David De Gea kwa mara nyingine kwani inasemekana klabu ya Real Madrid wameona ni ngumu sana kumnunua golikipa huyo na wameamua kuachana na mpango huo.

Baada ya kuweka wazi kwamba mwishoni mwa msimu huu ataondoka Real Madrid sasa mlinzi wa kati wa timu hiyo Pepe inadaiwa kwamba huenda katika msimu ujao wa ligi tukamuona katika ligi kuu nchini Ufaransa ambako anakaribia kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya PSG.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte anajipanga kutoa kiasi cha pesa pamoja na mchezaji mmoja kwa Juventus ili kuweza kumpata Leonardo Bonucci, Conte atalazimika kuwapa Juventus kiasi cha euro 48m na Nemanja Matic ili kumnunua Bonucci, kama Chelsea hawatatoa mchezaji mchezaji itawabidi watoe euro 60m.

Michy Batshuayi ameweka wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu ya Chelsea baada ya kukosa nafasi ya kucheza “kila mtu anajua kombe la dunia linakaribia na nahitaji muda mwingi kucheza ili kujiweka fiti na mashindano hayo, siwezi kutaka chochote hilo namwachia kocha ila ni bora niende nitakapopata muda wa kucheza”

Steven Gerrard kwa mara ya kwanza kwamba ilikuwa imebaki kidogo tu angejiunga na kocha Jose Mourinho, Gerrard amesema  kuna nyakati wakati Jose Mourinho alipokuwa akiifundisha Chelsea na baadae wakati anaifundisha Real Madrid alikaribia kujiunga na kocha huyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here