Home Kimataifa Waghana wamshukuru mungu kwa kombe la EPL

Waghana wamshukuru mungu kwa kombe la EPL

3346
0
SHARE

Hakika soka ni mchezo wa kusisimua sana,misismko,furaha,machozi na huzuni katika soka ni kati ya mambo ambayo yanaufanya mchezo huu kuonekana mchezo bora sana na wenye raha iliyopitiliza.

Mashabiki wa soka wamekuwa kama familia moja kwani kupitia soka tumekuwa tukikutana na watu wapya kila siku na kuifanya familia ya soka kuendelea kukua.

Baada ya Chelsea kuchukua ubingwa wa Uingereza katika msimu wa ligi ulioisha siku chache zilizopita, kanisa moja nchini Ghana limeutumia ubingwa huo kuzungumza na mwenyezi mungu.

Mchungaji wa kanisa hilo ambaye pia ni mshabiki wa kutupwa wa Chelsea aliamua kuwaita waumini huku wakiwa wamevaa jezi zao za Chelsea ili kukata keki,kufurahia ubingwa wao na pia kumuabudu mungu.

Siku ya ibada hiyo madhabahuni palijengwa kwa mtindo wa uwanja na wakati wa misa ikiendelea mchungaji Azigiza alimtania mchungaji mwenzake ambaye ni mshabiki wa Arsenal kuhusu ukame wa kombe la Epl unaiokumba Arsenal.

Katika ibada hiyo kuna wakati waumini ambao ni mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wakiimba nyimbo za Chelsea kwa furaha na baadae ibada iliendelea na kumuomba mungu kama kawaida.

Mchungaji wa kanisa hilo alilizungumzia tukio hilo na kusema wamefanya hivyo kutokana na nguvu ya mchezo wa soka ndipo wao wakaamua kuitumia nguvu hiyo kuongea na mwenyezi mungu.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here