Home Kimataifa Wachezaji wamlilia Cheikh Tiote.

Wachezaji wamlilia Cheikh Tiote.

11037
0
SHARE

Hakika atakumbukwa, alikuwa mtu wa mungu na alikuwa kwenye mfungo wa Ramdhan wakati mauti ilipomkuta, Cheikh Tiote kiungo ambaye nashukuru mungu nimeweza kushuhudia akicheza.

Nilivutiwa sana na Tiote hadi wakati Fellaini anajiunga na Manchester United nilitamani pengine labda Tiote ndiye angeenda United na sio Fellaini kutokana na ubora wake.

Baada ya kifo chake hapo jana baadhi ya wachezaji maarufu wameshindwa kuficha hisia zao na kuamua kumlilia Tiote kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Yohan Cabaye ambaye alicheza pamoja na Tiote wakati yuko Newcastle amesema kwamba anakosa hata uwezo wa kuongea kwani kifo hicho kimemuacha katika hali ya uchungu sana.

“Mungu akuangalie huko uliko,maneno yameshindwa kuelezea huzuni niliyonayo moyoni kuhusu wewe,hakika tutakukumbuka Cheikh Tiote” aliandika Cabaye.

Naye mlinzi wa kushoto wa Crystal Palace Andros Townsend amekiri kwamba Tiote ni kati ya watu poa sana na wachangamfu kuwahi kukutana nao katika maisha yake ya soka.

“Ni habari mbaya sana kuhusu Tiote,ni kati ya watu poa sana kuwahi kukutana nao, tutakukumbuka sana Tiote” aliandika Towmsend katila ukurasa wake wa Twitter.

Naye Didier Drogba ambaye ameshawahi kucheza timu moja na Townsend amesema hawezi kusema chochote kuhusu Tiote kwani ni habari iliyomchanganya sana.

Yaya Toure ameandika “kaka yangu Tiote siamini kama umeondoka hakika sitaweza kukusahau” huku Mohamed Salah akiandika “pumzika kwa amani Tiote”

Mchezaji nguli wa zamani wa Uingereza na Newcastle Alan Shearer ameleza pia kushtushwa na kifl cha Cheikh Tiote huku golikipa Rob Elliot akimtaja Tiote kama shujaa.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here