Home Kimataifa Kumbe tayari Romelu Lukaku anajua wapi anaenda

Kumbe tayari Romelu Lukaku anajua wapi anaenda

7451
0
SHARE

Lukaku ni kati ya majina ambayo yanatawala sana vichwa vya habari, hilo linatokana na uwezo wake lakini pia kwa jinsi vilabu mbalimbali vinavyopambana kumnunua Mbelgiji huyo.

Manchester United na Chelsea ndio vilabu ambavyo inasemekana vinakaribia kumnunua Lukaku na wote wanapewa nafasi kubwa katika usajili huo.

Wakati wa mchezo kati ya Ubelgiji na Czech Republic unachezwa kulikuwa na kundi la waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiria Lukaku atoke uwanjani ili wamhoji.

Baada ya muamuzi kupuliza filimbi ya mwisho katika mchezo huo ambao Ubelgiji walishinda mabao mawili kwa moja ndipo waandishi walimuuliza kuhusu nini kinaendelea katika uhamisho wake.

Lukaku amekiri kuna mazungumzo yanaendelea baina ya wakala wake na timu ambazo zinamuhitaji na pia anajua nini kinaendelea ila kwa sasa anachosubiri ni makubaliano tu yakamilike.

“Ninajua kinachoendelea ila namuachia Raiola amalize kila kitu akishamaliza tutafanya maamuzi yetu,nataka kucheza Champions League na kushinda Epl”

Katika msimu uliomalizika wa Epl Lukaku aliibuka katika nafasi ya pili ya ufungaji bora akiwa amefunga mabao 25 nyuma ya Harry Kane aliyefunga 29.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here