Home Kimataifa Habari za usajili Ulaya zinazovuma.

Habari za usajili Ulaya zinazovuma.

10258
0
SHARE

Klabu ya Arsenal tayari wameshaanza mapema kufanya usajili baada ya kumnunua Sead Kolasanic mlinzi wa kushoto wa klabu ya Schalke 04, Kolasanic amesaini bure Arsenal baada ya mkataba wake na Schalke kuisha.

Huko Hispania klabu ya Real Madrid haiwezi kumpa tena mkataba mlinzi wao wa kati Pepe, na hii itamfanya Pepe kuondoka Santiago Bernabeu ambapo ameishi kwa miaka 10.

Ujerumani nako klabu ya Borussia Dortmund imethibitisha kwamba wamepata kocha mpya, Petr Bosz aliyekuwa Ajax hapo mwanzo na sasa ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo na amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha klabu hiyo.

Ufaransa nako habari zinasema kuna vilabu kutoka nchini Uingereza vimetuma ofa ya zaidi £100m kumnunua Kylian Mbappe, vilabu vya Chelsea na Arsenal vimekuwa vikizungumziwa kumtaka mfunga mabao huyo.

Klabu ya Manchester City nayo inaendeleza fujo zake katika usajili na safari hii wamepiga hodi katika klabu ya Southampton ili kujaribu kumchukua mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Ryan Bertrand.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here