Home Kimataifa Cheikh Tiote hatunaye tena.

Cheikh Tiote hatunaye tena.

2815
0
SHARE

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Everton Cheikh Tiote amefariki dunia,Tiote amefariki nchini China ambako alikuwa akiitumikia klabu ya Beijing Enterprises ya nchini humo.

Tiote alijiunga na klabu ya Beijing baada ya kuitumikia klabu ya Newcastle kwa muda wa miaka saba kabla ya mwezi January kujiunga na klabu hiyo ya China.

Inasemekana Tiote mwenye umri wa miaka 30 alipatwa na shambulio la moyo akiwa mazoezini na baada ya kupelekwa hospitali ndiko alipumua pumzi yake ya mwisho.

Emmanuele Palladino ambaye ni wakala wa Tiote amethibitisha taarifa hizo “nathibitisha taarifa za mteja wangu kufariki baada ya kuanguka alipokuwa mazoezini leo asubuhi”

Cheikh Tiote ukiachilia mbali kuwa mchezaji wa Newcastle lakini aliitumikia pia timu ya taifa ya Ivory Coast akishinda michezo 52 na alikuwepo katika kombe la dunia la mwaka 2010 na 2014.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here