Home Dauda TV Video: Matuta yaliyoipeleka Yanga nusu fainali michuano ya SportPesa

Video: Matuta yaliyoipeleka Yanga nusu fainali michuano ya SportPesa

15168
0
SHARE

Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia timu hizo kumaliza dakika 90 kwa matokeo ya suluhu.

Shujaa wa mchezo alikuwa golikipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ ambaye alifanikiwa kupangua penati moja ya Clifford Alwanga huku penati ya Stephen Owusu ikigonga mwamba wa juu na kutoka nje.

Yanga walikwamisha penati nne kambani huku Tuster wakifanikiwa kufunga mikwaju miwili na kutupwa nje ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Matuta ya Yanga yamefungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyefunga penati ya kwanza akifuatiwa na Obrey Chirwa, kisha Maka Edward Mwakalukwa na Said Mussa wakafunga penati zao.

Kwa upande wa Tusker, waliofanikiwa kufunga mikwaju ya penati ni Noah Wafula na Brian Osumba.

Matokeo hayo yataikutanisha Yanga na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here