Home Kimataifa Griezman agongelea msumari wa moto katika kidonda cha Manchester United.

Griezman agongelea msumari wa moto katika kidonda cha Manchester United.

5907
0
SHARE

Yametimia, hakika unaweza kusema tu hivyo japokuwa hujui ni nini kitatokea kesho kwani lolote linaweza kutokea haswa pale palipo na pesa.

Antoine Griezman tetesi zimekuwa ndefu sana,huyu akisema lile na yule akisema hili kuhusiana na uhamisho wake wa kwenda Manchester United.

Griezman mwenyewe alisema wazi kwamba kuna alama 6 kati ya 10 kwamba yeye anakwenda United na kuifanya dunia iamini kwamba kweli Griezman anatua Old Trafford.

Lakini tweet ya mchezaji huyo imebadilisha kabisa upepo wa habari yake na kuanza kuipeleka katika upande mpya kwani Griezman anaonekana kubaki Atletico Madrid.

Griezman aliandika “now more then ever” na kuweka hashtags ambazo zilionesha umoja alionao yeye na klabu yake ya sasa ya Atletico Madrid.

Taarifa toka ndani ya klabu ya Manchester United zinasema United tayari wameona dili hilo ni gumu kwa sasa na wameanza kuangalia uwezekano wa nyota mwingine mkubwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here