Home Dauda TV Video: Jafar Idd amewataja wachezaji waliotemwa Azam

Video: Jafar Idd amewataja wachezaji waliotemwa Azam

25603
0
SHARE

Klabu ya Azam mbali na kukanusha kuhusu Manuala kuiacha klabu hiyo na kujiunga na Simba, wamezungumzia mambo mengine matatu yanayoihusu klabu yao.

Mambo yaliyozunguzwa na Azam ni pamoja na kutoa orodha ya wachezaji walioachwa na klabu hiyo baada ya kumaliza mikataba, wachezaji wa timu ya vijana waliopandishwa kucheza timu ya wakubwa pamoja na mipango ya usajili.

Ame Ally ‘Zungu’, Hamisi Mcha ni miongoni mwa wachezaji waliotemwa katika awamu ya kwanza lakini Jafar Idd amesema kuna awamu nyingine ambayo pia huenda wachezaji kadhaa wakatoswa na klabu hiyo.

Jafar amewataja wachezaji watano waliopandishwa timu ya wakubwa wakitokea timu ya vijana (U20).

Amezungumzia pia kuhusu mipango ya usajili na nafasi ambazo wataziangalia kutokana na mapendekezo ya kocha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here