Home Kitaifa Shaffih Dauda vs Edgar Kibwana kuhusu Azam kumtema Saad Kawemba

Shaffih Dauda vs Edgar Kibwana kuhusu Azam kumtema Saad Kawemba

8914
0
SHARE

Juni 1, 2017 Azam ilitoa taarifa rasmi kuhusu kuachana na mtendaji wao mkuu Saad Kawemba baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi kuamua kuachana nae pamoja na kuifuta nafasi ya mtendaji mkuu (C.E.O) kwenye klabu yao.

Mijadala imekuwa mingi na mikali kuhusu hatua ya Azam kuachana na Kawemba na kuifuta nafasi aliyokuwa anaitumikia, ndani ya Sports Extra kulikuwa na mjadala mkali ambapo wachambuzi wa kituo hicho Shaffih Dauda na Edgar Kibwana nao walipishana mitazamo kuhusu hatua ya Azam.

Kibwana yeye bado anaona kuna ukakasi katika uamuzi uliofanywa na Azam kuhusu kuifuta nafasi ya mtendaji mkuu huku pointi yake ya msingi ikiwa ni kwamba, wakati Azam wanamwajiri Abdul Mohamed kama General Manager  hawakujua kama tayari walikuwa na C.E.O? Hakuna tofauti ya kiutendaji kati ya C.E.O na General Manager? Majukumu aliyokuwa anayatekeleza Kawemba yatafanywa na nani?

“Napata mashaka na utendaji wa Azam FC, sijui wanata nini. Wamemuondoa Saad Kawemba kama C.E.O wa Azam FC na kukifuta kabisa cheo hicho, wakati wanamuajiri Abdul Mohamed kama General Manager hawakutambua kuwa kulikuwa na C.E.O? Walihitaji nini kutoka kwa Kawemba na Abdul?, “ amesema Edgar Kibwana.

Kwa upande wake Shaffih Dauda yeye hakuwa tofauti na uamuzi uliofanywa na Azam, amesema kuondoka kwa Kawemba ni sawa na kumpa meno Abdul Mohamed kwa sababu awali majukumu ya wawili hao yalifanana na kulazimika kugawana ili tu kila mmoja aonekane anawajibika.

“Mimi nimewaelewa sana Azam kwa kumuondoa Saad Kawemba pamoja na kuifuta nafasi ya C.E.O ndani ya klabu yao kwa sababu Kawemba na Abdul Mohamed majukumu yao yalikuwa yanafanana.”

“Ilibidi wagawane majukumu ili kila mmoja aonekane anafanya kazi, Kawemba akawa yupo zaidi kwenye mambo ya kiutawala halafu Abdul akabaki kupambana na mambo yanayoihusu timu tu lakini kiuhalisia ni majukumu ambayo yangeza kufanywa na mtu mmoja.”

“Kuondoka kwa Saad Kawemba ni sawa na kumpa meno Abdul Mohamed ambaye awali alikuwa anatembea juu ya kivuli cha Kawemba.”

Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na mitazamo mingi kuhusu jambo hili, naomba comment yako kuhusu mtazamo wako juu ya Azam kuachana na Kawemba na kuifuta nafasi ya C.E.O. Je wako sahihi na watafanikiwa au wamechemka?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here