Home Dauda TV ‘Manula haendi timu yoyote Tanzania’ – Azam

‘Manula haendi timu yoyote Tanzania’ – Azam

11997
0
SHARE

Wakati kukiwa na taarifa kwamba golikipa tegemeo wa Azam FC Aishi Manula ameshamwaga wino kuitumikia klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili, afisa habari wa Azam Jafar Idd amesema golikipa huyo ataendelea kubaki Azam.

Jafar amesema, mazungumzo kati ya manula na uongozi wa Azam yanakwenda vizuri na kinachosubiriwa ni kukamilisha baadhi ya taratibu baada ya golikipa huyo wa Stars kurejea nchini kutoka Misri ambako yupo kambini na timu ya taifa.

“Aishi Manula na Shomari Kapombe mazungumzo yao na Azam yapo katika dakika za mwisho na yanakwenda vizuri, Aishi Manula ataendelea kuwepo Azam FC. Kilichobaki tunasubiri wakirudi kutoka Misri waje wakamilishe taratibu na uongozi. nawatoa shaka mashabiki wa Azam kuhusu suala la Manula kwamba bado ataendelea kuwepo Azam.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here