Home Kimataifa UCL Final: Kwanini Madrid italipa zaidi ya billion 200 kwa kutwaa Champions...

UCL Final: Kwanini Madrid italipa zaidi ya billion 200 kwa kutwaa Champions League vs Juve

23463
0
SHARE

Yamebaki masaa takribani 48 kabla ya referee wa kijerumani Felix Brynch hajapuliza kipenga cha kuashiria kuanza kuanza kwa mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya msimu wa 2016/17.


Jijini Cardiff, Real Madrid watakuwa wanautafuta ubingwa wa 12 wa ulaya wakati watakapopambana na Juventus – lakini pia ubingwa huu wataigharimu klabu zaidi ya billioni 200 za kitanzania kwa ajili ya bonasi za kulipa wafanyakazi wao.

Haijawahi kutokea katika historia ya kizazi hiki kwa timu yoyote kuweza kutetea ubingwa wa ulaya, lakini vijana wa Los Blancos sasa wana sababu zaidi ya moja kuiweka rekodi mpya.

Nahodha Sergio Ramos na wachezaji wenzake wakubwa katika klabu hiyo walicheza kamari wakati walipojadili juu ya maombi ya bonasi, na klabu ilikubali maombi yao na sasa wanahitaji kuifunga Juve ili warudi Madrid wakienda bank wanacheka.

Wakati ilipoonekana kuna uwezekano wa Real kushinda makombe mawili msimu huu, ilkubaliwa kwamba kila mchezaji atapokea 1.5 millioni euros kwa kufanikisha mafanikio hayo.

Msimu uliopita, klabu ililipa jumla ya 32 million euros kwenye bonasi za wachezaji na benchi la ufundi, hii ilitokana na ushindi wa Champions League na kila mmoja alivuta takribani kiasi cha  700,000 euros per na 100,000 euros kwa kuifunga Barcelona pale Camp Nou katika El Clasico.

Wakati huu, Los Blancos chini Florentino Perez wanatarajiwa kulipa kiasi cha zaidi ya 80 million euros ambazo kwa pesa ya madafu ni zaidi ya 208 billion – lakini tu endapo wataifunga Juventus katika mchezo wa fainali ya Mabingwa wa ulaya usiku wa Jumamosi ya tarehe 3 June.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here