Home Dauda TV Exclusive: Dauda TV imemnasa mchezaji wa zamani wa Everton

Exclusive: Dauda TV imemnasa mchezaji wa zamani wa Everton

5351
0
SHARE

Dauda TV imemnasa mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman ambaye kwa sasa ni balozi wa klabu hiyo, Osman kwa sasa yupo nchini ikiwa ni utangulizi kabla ya ujio wa klabu ya Everton nchini mwezi July, 2017.

Amezungumza mambo mengi kuhusu wakati wake akiwa kama mchezaji wa Everton lakini pia hakuacha kugusia kuhusu ziara ya klabu hiyo nchini na Afrika kwa ujumla.

Amesema ujio wao Tanzania utawasaidia katika kujitangaza na kutengeneza mashabiki wengi katika bara la Afrika.

“Ni hatua nzuri kwa klabu kujitangaza duniani hususan kwenye bara la Afrika na miaka michache ijayo Everton itakuwa ni miongoni mwa vilabu maarufu duniani.”

Kuhusu klabu ambayo ilimpa wakati mgumu kipindi anacheza EPL, Osman amesema alikuwa anafurahia zaidi kucheza dhidi ya West Ham United.

“Kuna vilabu vingi ndani ya Premier League ambavyo vinaupinzani mkubwa sana mkicheza dhidi yao lakini nilikuwa nina-enjoy kucheza na West Ham United kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa sababu nilikuwa nafunga magoli dhidi yao.”

 

“Nilikuwa pia napenda kucheza kwenye uwanja wa White Hart Lane, lakini nilikuwa napenda ushindani uliokuwepo dhidi ya West Ham.”

Balozi huyo wa Azam amesema, wakati wa uchezaji wake Ashley Cole alikuwa anampa changamoto ukilinganisha na wachezaji wengine aliokuwa anakutana nao.

“Mlinzi wa zamani wa kushoto wa England na vilabu vya EPL vya Arsenal na Chelsea Ashley Cole ni mchezaji ambaye alikuwa ananipa changamoto nilipokuwa nikikutana nae, alikuwa ana nguvu na kasi.”


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here