Home Kitaifa Mbaraka hana tatizo na Simba, kamilisheni mahitaji yake

Mbaraka hana tatizo na Simba, kamilisheni mahitaji yake

13758
0
SHARE

Mshambuliaji wa Kagera Sugar na timu ya taifa Mbaraka Yusuph amesema yupo tayari kurudi Simba endapo klabu hiyo itatimiza mahitaji yake kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia.

“Nipo tayari kurudi Simba endapo watakidhi mahitaji yangu,” amesema Mbaraka wakati akizungumza na Sports Extra ya Clouds FM.

Mbaraka alitolewa kwa mkopo kwenda Kagera Sugar, lakini baada ya mkataba wake na Simba kumalizika akajiunga na Kagera Sugar ambayo inammiliki kama mchezaji wao halali tofauti na Simba wanavyodai kwamba bado ni mchezaji wao halali.

“Mimi ni mchezaji halali wa Kagera Sugar, mkataba wangu na Simba ulishamalizika kwa hiyo kama wananihitaji inabidi tukae chini na kuzungumza.”

Mbaraka amesema malengo yake katika msimu uliopita yalikuwa ni kuwa mfungaji bora lakini hakufanikiwa badala yake akaishia kufunga magoli 12 magoli mawili nyuma ya Simon Msuva na Abdulrahman Musa walioshinda tuzo hiyo kwa kufunga magoli 12 kwa msimu mzima.

“Nilipanga niwe mfungaji bora msimu huu lakini kwa bahati mbaya malengo yangu hayajatimia, nashukuru kwa hii tuzo niliyoshinda ya mchezaji bora chipukizi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here