Home Kitaifa ‘Kama waamuzi watatenda haki, timu yoyote inaweza kuchukua ubingwa’ – Aishi Manula

‘Kama waamuzi watatenda haki, timu yoyote inaweza kuchukua ubingwa’ – Aishi Manula

14739
0
SHARE

Golikipa wa Azm FC na Taifa Stars Aishi Manula amesvunja ukimya na kusema, endapo waamuzi wa Tanzania watachezesha mechi za mashindano mbalimbali basi timu yoyote inaweza kuibuka bingwa mbali na timu zenye majina makubwa kama Azam, Simba na Yanga.

“Kama waamuzi wa ligi yetu watatenda haki, timu yoyote inaweza kuchukua ubingwa,” amesema Manula ambaye ni mshindi wa tuzo ya golikipa bora VPL 2016/2017.

Manula amesema, Azam, Yanga na Simba hazifanyi vizuri kimataifa kwa sababu ya upendeleo zinaopewa na baadhi ya waamuzi wa ndani.

“Azam, Simba na Yanga hazifanyi vizuri kimataifa kwa sababu zinapata ‘favor’ kwenye ligi ya ndani.”

Manula ameamua kung’oa kabisa mzizi wa fitina kuhusu soka la Bongo hakuacha kumpongeza mwamuzi bora wa VPL 2016/2017 Elly Sasii.

“Tukipata waamuzi kama aliyeshinda tuzo ya mwamuzi bora msimu huu (Elly Sasii) tutafika mbali.”

Golikipa huyo anaekuja kwa kasi hakuacha kusema kwamba, wadau wengi wanafatilia timu chache za ligi na kugundua makosa machache ya waamuzi lakini zinapocheza timu zenye majina madogo ndipo yanapofanyika madudu lakini watu hawaoni kwa sababu hawafatilii.

“Watu wanafatilia timu chache tu zinazocheza ligi, lakini zinapocheza timu ambazo hazina majina ndio yanafanyika ‘madudu’ mengi lakini watu hawajui kwa sababu hawafatilii.”

“Ukisikia mwamuzi kafungiwa basi itakuwa kwa sababa ameharibu kwenye mechi inayozihusisha timu za Azam, Yanga au Simba. Huwezi kusikia mwamuzi kafungiwa kwenye mechi ya Ndanda na African Lyon, lakini huku ndio kwenye madudu mengi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here