Home Dauda TV Video: Shabiki wa Simba aliyekemea ‘mapepo’ kabla ya Simba kubeba kombe la...

Video: Shabiki wa Simba aliyekemea ‘mapepo’ kabla ya Simba kubeba kombe la ASFC

5833
0
SHARE

Katika mchezo wa soka kuna mambo mengi ambayo yanachangia timu kushinda licha ya kuwa na kikosi au wachezaji wanacheza vizuri ndani ya uwanja, hamasa ya nje ya uwanja husaidia timu kufanya vizuri.

Kwenye fainali ya Kombe la shirikisho (FA Cup) iliyofanyika mkoani Dodoma alikuwepo shabiki ambaye alikuwa na hamasa iliyosaidia kuwapa Simba ubingwa na Dauda Tv ilipata nafasi ya kuzungumza naye.

Ahazi Sadock Mwembe huyu ni shabiki wa Simba kutoka Tunduma, Songwe. Ubunifu wake aliokuja nao kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma ulikuwa kivutio na kiburudisho tosha ukiachana na mambo mengine ya pembeni.

Kabla ya mechi ya fainali ya ASFC kati ya Simba vs Mbao aliiombea Simba kwa kukemea mapepo ili klabu yake iibuke na ushindi dhidi ya Mbao na kuchukuoa kombe, na baada ya mechi kumalizika Simba ndio walikuwa washindi kufuatia kuifunga Mbao mabao 2-1 na kutwaa taji la ASFC 2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here