Home Kimataifa Kwaheri Fransesco Totti, atundika daluga rasmi Roma ikiibuka kidedea

Kwaheri Fransesco Totti, atundika daluga rasmi Roma ikiibuka kidedea

1969
0
SHARE

Alikuwa na miaka 16 tu mwaka 1993 wakati anavaa jezi ya Roma lakini tarehe 28 siku ya Jumapili akiwa na miaka 40 amechoka anavua jezi na kuamua kupumzika.

Huyo ni Francesco Totti moja kati ya washambuliaji bora sana wa Kiitaliano kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka na kila siku atakuwa katika mioyo ya mashabiki wa As Roma.

Katika mchezo ambao As Roma waliifunga Genoa mabao 3 kwa 2, machozi na simanzi yalionekana kutawala uwanjani wakati wa kumuaga Francesco Totti.

Totti ambaye amewahi kushinda kombe la dunia mwaka 2006 aliwahi pia kushinda kikombe cha Serie A na katika michezo 783 aliyoicheza amefunga jumla ya mabao 307.

Msimu huu Totti ameichezea As Roma michezo 27 lakini karibia yote alikuwa akitokea benchi na kuisaidia Roma kumaliza nafasi ya pili wakiwa na alama nne nyuma ya mabingwa Juventus.

Tayari klabu hiyo ya Italia imeamua kumpa nafasi mpya Totti ambapo ataanza kuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo kazi ambayo anaianza rasmi siku ya Jumatatu.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here