Home Kitaifa Exclusive: Ukweli kuhusu Ibrahim Ajibu kusaini Singida United

Exclusive: Ukweli kuhusu Ibrahim Ajibu kusaini Singida United

35720
0
SHARE

Jana Mei 28, 2017 kulikuwa na taarifa inasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu klabu ya Singida United kumalizana na mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib huku kukiwa na wachezaji wengine wawili wakitarajiwa kujiunga na klabu hiyo iliyopanda daraja kucheza VPL msimu ujao.

shaffihdauda.co.tz imemtafuta Festus Sanga ambaye ni Mkurugenzi wa klabu hiyo ili kupata ufafanuzi kuhusu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kama kinaukweli.

“Bado hatujamalizana na Ajib lakini tupo naye kwenye mazungumzo na kila kitu kinakwenda vizuri kama tutafikia makubaliano tutamsajili kwa ajili kuitumikia klabu yetu kuanzia msimu ujao,” amesema Festus Sanga.

“Ajib anamalizia mkataba wake kwenye klabu yake ya sasa (Simba) kwa hiyo ana ofa nyingi kutoka vilabu mbalimbali kwa hiyo tunahitaji kumshawishi ili akubali kujiunga na sisi.”

Jumamosi Mei 27, 2017, Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba alionekana akiwa amevaa jezi ya Simba yenye jina la Ajibu mgongoni. Mh. Nchemba ni mlezi wa klabu ya Singida United lakini pia ni shabiki wa ‘lialia’ wa Yanga.

Mh. Nchemba kuvaa jezi ya Ajibu kunatoa ishara fulani kuhusu Ajibu kujiunga na Singida United.

Juma lililopita, klabu ya Singida United ilimsaini Kenny Ally kutoka Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here