Home Kimataifa Manchester United wabeba ubingwa na kukata tiketi ya Champions League

Manchester United wabeba ubingwa na kukata tiketi ya Champions League

6248
0
SHARE

Ilikuwa ni kufa au kupona kwani United wasingeshinda mchezo wao wa fainali dhidi ya Ajax baasi wangepoteza nafasi ya kushiriki michuano ijayo ya champions league.

Japokuwa Ajax walionekana kama wanaweza kufanya jambo la tofauti katika mchezo huo kutokana na walivyoonekana kuwashika Manchester United lakini uzoefu uliwamaliza. United wamechukua kombe hilo na limemfanya Jose Mourinho sasa kuwa na vikombe vinne vikubwa michuano ya Ulaya.

Dakika ya 18 tu mchezaji ghali kwa Manchester United kiungo Paul Pogba alizifumania nyavu za Ajax na kuufanya mchezo huo kwenda half time United wakiongoza kwa bao moja, Pogba hii ni mara yake ya kwanza kufunga mechi mbili mfululizo tangia afanye hivyo mwezi April mwaka jana.

Kipindi cha pili Ajax walionekana kupambana wakijaribu kusawazisha bao hilo lakini dakika ya 48 tu waliruhusu tena nyavu zao kuguswa na Mualmernia Henrikh Mkhtaryan baada ya kuandika bao la pili, Mkhitaryan mabao 6 ya mwisho kuifungia United yote ameyafunga katika michuano hii.

Mchezo huo ulimalizika hivyo na kuifanya United kwa mara ya kwanza kushinda kombe hilo ambalo lilikuwa ndio kombe pekee ambalo hawajawahi kuchukua. Matokeo hayo pia yanaipa Manchester United tiketi ya kushiriki champions league msimu ujao.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here