Home Kitaifa Vipigo vya ‘heavy weight’ VPL 2016/2017

Vipigo vya ‘heavy weight’ VPL 2016/2017

6962
0
SHARE

Ligi kuu Tanzania bara imemalizika weekend iliyopita na Yanga kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo huku likiwa ni taji lao la 27 katika historia.

Baada ya ligi kumalizika kilichobaki ni kuangalia mambo mbalimbali yaliyojiri katika kipindi chote cha pilikaza msimu huu. Leo tunaanza kwa kuangalia timu zilizotoa vipigo vikubwa katika msimu huu.

Yanga

Ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba ndio ushindi mkubwa katika msimu huu. Ushindi huo ulipelekea kusimamishwa kwa golikipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ wa Kagera kwa madai ya rushwa.

Yanga ndio timu inayoongoza kwa kugawa dozi nzitonzito msimu huu, JKT Ruvu walichezea 4-0, Ndanda baada ya kukomaa kwao na kulazimisha suluhu walivyotua Dar wakala 4-0.

Stand United waliifunga Yanga 1-0 uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, walivyokanyaga Dar kipigo cha mabao 4-0 kiliwahusu.

Mbao FC

Ukiwa ni msimu wao wa kwanza kucheza VPL katika historia yao, waliipiga Mtibwa Sugar kwa bao 5-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba mwanza na kuwashtua wengi kutokana na Mtibwa kusheheni wachezaji wazoefu wa ligi wenye majina makubwa na wengine walipata kucheza katika vilabu vikubwa nchini vya Simba na Yanga.

Mbao ili kudhihirisha wao si wa mchezomchezo waliwakalisha Ruvu Shooting kwa kuwapa kisago cha magoli 4-1 na kudhihirisha kwamba hawakubahatisha kuigaragaza Mtibwa.

Simba

Ushindi mkubwa wa Simba msimu huu iliupata dhidi ya Majimaji, baada ya kuibugiza goli 4-0 kwenye uwanja wa taifa. Baada ya hapo Simba haikushinda tena kwa magoli zaidi ya matatu hadi msimu ulipomalizika.

Azam FC

Haukua msimu mzuri sana kwao, wamebadili mabenchi mawili ya ufundi katika msimu mmoja lakini bado haikusaidia kuwafanya wafanye vizuri katika msimu.

Ushindi wao wa magoli 4-1 dhidi ya Mwadui ugenini ni miongoni mwa mechi zilizotoa vipigo vikali katika msimu huu ambao umemalizika.

Mbeya City

Walipata ushindi wao mkubwa msimu huu dhidi ya Mbao pale walipoitandika kwa magoli 4-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kuondoka na pointi tatu muhimu.

Ruvu Shooting

Wakiwa ugenini, timu hiyo inayomilikiwa na jeshi la kujenga taifa kutoka mkoa wa Pwani ilijipigia Majimaji kwa bao 4-1 na kumpa fursa msemaji wao Masao Bwire kutamba kila kona kutokana na ushindi mnono.

Mtibwa Sugar

Mtibwa nao walifanikiwa kutoa kichapo cha magoli 4-2 dhidi ya Mwadui kwenye uwanja wa Manungu Complex uliopo katikati ya mashamba ya miwa huko Turiani, Morogoro.

Mwadui FC

Baada ya kuchezea vipigo vya mabao 4 kutoka Azam na Mtibwa, Mwadui wakajipumzisha kwa Ndanda kwa kuaangushia kipondo cha magoli 4-2 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here