Home Kimataifa Vidal atoa siri iliyoko kati ya Bayern Munich na Alexis Sanchez.

Vidal atoa siri iliyoko kati ya Bayern Munich na Alexis Sanchez.

6347
0
SHARE

Misimu ya ligi kuu karibia zote duniani umekwisha, wachezaji wanakwenda kupumzika huku wengine wakisubiria fainali za Ulaya na baadhi ya makombe nchini mwao.

Wakati wa mapumziko pia ndio wakati wa kujiandaa na msimu ujao ambapo timu mbali mbali hutumia muda huo kuanza kuboresha vikosi vyao.

Arsenal wako katika hatihati za kumpoteza mchezaji wao bora zaidi Alexis Sanchez, taarifa zinadai Juventus, Chelsea na PSG wanamtaka baada ya kushindwana na Arsenal.

Wakati timu hizo zikipambana kumnunua Sanchez, taarifa mpya zimeibuliwa na kiungo wa klabu ya Bayern Munich Artulo Vidal kwa kusema klabu hiyo inamfuatilia sana Sanchez.

Bayern ambao ni mabingwa wa ligi ya Ujerumani wamekuwa wakimuuliza Vidal ambaye anatokea taofa moja na Sanchez kuhusu uwezo wa mchezaji huyo na maisha yake kwa ujumla.

“Mara zote walizonifuata kuniuliza kwamba ni mchezaji wa aina gani, niliwaambia ni mchezaji ambaye hakika anapaswa kuja Bayern, mkataba wake umebaki mwaka mmoja Arsenal naamini anaweza kuletwa” alisema Vidal.

Vidal anaamini Sanchez ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu na anapswa kufanya maamuzi kwa ajili yake na kwa ajili ya taifa lao la Chile kwani wanamtegemea.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here