Home Kitaifa Malinzi kamaliza utata tuzo ya mfungaji bora VPL 2016/17

Malinzi kamaliza utata tuzo ya mfungaji bora VPL 2016/17

22294
0
SHARE

Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake rasmi wa twetter amesema, Simon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting) watapata zawadi sawa ya ufungaji bora baada ya wawili hao kufungana kwa idadi ya magoli hadi mwisho wa ligi.

Wote wawili wamefanikiwa kufunga magoli 14 na hapo ndipo ikaanza kuibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nani atakae stahili kupewa tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu kwa msimu huu 2016/2017.

Kwa kuwa vijana wrtu Abdlrahman Musa na Simon Msuva wamefunga idadi sawa ya mabao (14) VPL, wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa Tsh. 5.8m,” ameandika Malinzi.

Sherehe ya ugawaji wa tuzo za VPL 2016/2017 zitafanyika Mei 24, 2017 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here