Home Ligi EPL Unamshangaa Kante kubeba ubingwa? Ona hawa wengine.

Unamshangaa Kante kubeba ubingwa? Ona hawa wengine.

9874
0
SHARE

Ngolo Kante kati ya bahati alizonazo ni kubena ubingwa msimu uliopita na msimu huu akiwa na timu mbili tofauti, lakini wapo wengine ambao wameshabeba Epl na timu mbili tofauti.

Ashley Cole. Wakati Ashley Cole alipokuwa na Arsenal alishinda kombe hilo mara mbili ikiwa ni mwaka 2004 na 2002, baadaye Cole alihamia Chelsea ambako nako alishinda kikombe hicho mwaka 2010.

Henning Berg.Berg alikuwa mchezaji wa zamani wa Blackburn na mwaka 1995 walifanikiwa kubeba kikombe cha ligi kuu akiwa na timu hiyo, baadaye Berg alihamia Manchester United na akabeba tena kombe hilo mwaka 1999 na 2000.

Carlos Teves.Teves alipokuja Uingereza alianza kukipiga na timu ya Manchester United ambapo chini ya kocha Alex Ferguson walifanikiwa kuchukua ubingwa mwaka 2008 na 2009 lakini baadae alihamia timu jirani ya Manchester City na akabeba kombe hilo mwaka 2012.

Kolo Toure.Toure mwanzo alikuwa akikipiga katika klabu ya Arsenal na akaisaidia kubeba ubingwa mwaka 2004, alipohamia Manchester City aliisaidia tena kubeba ubingwa mwaka 2012.

Nicolas Anelka.Kama ilivyo kwa Ashley Cole, Anelka naye ana historia inayofanana naye katika kubeba ubingwa, Anelka alianza kubeba kombe akiwa na Arsenal mwaka 1998 na akafanya hivyo tena na Chelsea mwaka 2010.

Gael Clichy.Arsenal wanaonekana kutawala katika orodha ya kuwapa wachezaji ubingwa kabla ya mwaka 2010 na kuendelea,  mwaka 2004 Clichy alibeba kombe na Arsenal lakini mwaka 2012 na mwaka 2014 akabeba tena na Man City.

Robert Huth.Msimu wa mwaka 2005 Huth alikuwa akiitumikia Chelsea na ndio alianza kuchukua nao kombe, baadae alihamia Leicester ambapo msimu wa mwaka 2015/2016 nako alichukua nao kombe.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here