Home Kitaifa Nadir mataji 8, Kelvin Yondan mataji 7, Kaseja mataji 6, hawa ndiyo...

Nadir mataji 8, Kelvin Yondan mataji 7, Kaseja mataji 6, hawa ndiyo wababe wa VPL

9363
0
SHARE

Na Barpaka Mbolembole

MLINDA mlango wa Kagera Sugar FC, Juma Kaseja alishinda mataji matano ya ligi kuu Tanzania Bara akiichezea Simba SC (2003, 2004, 2007, 2009/10 na 2011/12) na taji lingine moja akiichezea Yanga SC (2008/09).

Kaseja ni golikipa pekee aliyreshinda mataji mengi zaidi ya ligi kuu miongoni mwa wachezaji wanaokipiga katika VPL msimu huu.

Baada ya michezo ya kukamilisha msimu wa 2016/17 siku ya Jumamosi walinzi wa kati wa Yanga, Kelvin Yondan na nahodha Nadir Haroub wamejiwekea rekodi ya kushinda mara nyingi zaidi taji hilo. Wawili hao wametofautiana taji moja tu licha ya wote kuanza kucheza VPL msimu mmoja.

Kelvin ambaye alianza kucheza VPL mwaka 2006 akiwa Simba alifanikiwa kushinda mataji matatu ya VPL misimu ya 2007, 2009/10 na 2011/12. Mlinzi huyo wa zamani wa Taifa Stars alijiunga na Yanga katikati ya mwaka 2012 na kuanzia hapo amefanikiwa kushinda mataji manne ya VPL ndani ya misimu yake mitano. Aliisaidia Yanga kushinda ubingwa huo misimu ya 2012/13, 2014/15, 2015/16 na 2016/17.

Nahodha wa Yanga, Nadir ambaye alijiunga Yanga mwaka 2006 akitokea kwao Zanzibar amedumu klabuni hapo kwa misimu 11 sasa na kuisaidia klabu yake kushinda mataji 8 kati ya 27 ya kihistoria klabuni hapo.

Nadir alishinda ubingwa huo kwa mara ya kwanza mwaka 2006, akashinda tena msimu wa 2007/08, 2008/09, 2010/11, 2012/13, 2014/15, 2015/16 na 2016/17. Tangu kuanza kwa karne mpya Nadir anabaki kuwa mchezaji aliyeshinda mataji mengi zaidi ya VPL akifuatiwa na Kelvin na golikipa Juma Kaseja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here