Home Kitaifa Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2016/2017

12311
0
SHARE

Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kutetea ubingwa wake wa VPL msimu huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo tangu walipolitwaa taji hilo msimu wa 2014/15 hadi sasa 2016/17.

Licha ya kufungwa ugenini na Mbao FC kwa goli 1-0, bado kipigo hicho hakikuizuia Yanga kushinda taji hilo kutokana na wastani mzuri wa magoli waliokuwa nao dhidi ya mpinzani wao Simba.

Yanga walikua wanauhakika wa kulitetea taji lao baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Toto Africans mechi iliyochezwa Jumanne iliyopita kwenye uwanja wa taifa. Baada ya ushindi huo Yanga walifikisha pointi 68 na kuongoza ligi kwa taifauti ya pointi tatu dhidi ya Simba.

Baada ya ushindi wa mechi yake ya mwisho, Simba imefikisha alama 68 lakini ikapigwa bao na Yanga kutokana na wastani wa magoli. Yanga ina wastani wa magoli 43 huku Simba ikiwa na wastani wa magoli 33.

Simba imeendelea kuteswa na Yanga na Azam kwa sababu mara zote taji hilo limeenda Azam na Yanga tangu Simba walipilipoteza kwa mara ya mwisho. Mara ya mwisho Simba kutwaa taji hilo ilikuwa ni msimu wa 2012/13.

Ubingwa wa msimu huu (2016/17) ni wa 27 kwa Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here