Home Kimataifa Conte awafuata Neymar na Paul Pogba.

Conte awafuata Neymar na Paul Pogba.

17744
0
SHARE

Mitandao ya kijamii imeteka sana dunia na kila siku imekuwa ikitafuta sana njia mpya za kwa karibu na wafuasi wake kwa kubuni vitu vipa kila kukicha.

Mtandao wa Twitter umekuwa ukijaribu njia nyingi ili kuwa karibu na mashabiki wake haswa wale wapenzi wa michezo kama soka na micheO mingine maarufu.

Twitter siku chache zilizopita waliamua kuanzisha emoji kwa wachezaji wawili wakubwa, wakianza na Paul Pogba wa Manchester United na baadae Neymar wa Barcelona.

Baada ya Chelsea kubeba ubingwa gumzo kubwa limekuwa uwezo wa kocha wao Antonio Conte na kiungo Ngolo Kante ambao wanaonekana kama nguzo kubwa katika ubingwa huo.

Baada ya ubingwa huo Twitter wameamua kuja na kitu special kuhusu ubingwa huo ambapo wameamua kuanzisha emoji maalum kwa ajili ya kocha wa Chelsea Antonio Conte.

Sasa mashabiki wa Chelsea wanapaswa kuandika tu #ChelseaChampions na wakiandika hivyo kutakuja picha ndogo ya kocha wao huyo Muitaliano.

Chelsea watakuwa uwanjani siku ya Jumapili katika mchezo wao wa mwisho wa ligi ambapo ushindi katika mchezo huo utawafanya kufikia rekodi yao ya ushindi ya msimu wa 2004-2005 ambapo walishinda michezo 30.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here